Na Mwandishi wetu
Bukoba
ASKARI wawili wa jeshi la polisi wilaya ya Ngara mkoa
wa Kagera wameuawa baada ya kupigwa na wananchi wa kijiji cha Kasheshe
kata ya Rugu wilayani Karagwe.
Askari waliouawa
wametambuliwa kwa ni sajenti Thomasi Magiro na Koplo Damasi Kisheke
wote kutoka wilaya ya Ngara, majira ya
saa 5:30 usiku kijijini hapo.
Baada ya askari hao kuuawa gari walilokuwa nalo aina
ya Noha liliteketezwa kwa moto.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio wananchi walipoanza kuwashambulia askari hao, askari
mmoja wapo aliyekuwa na bunduki ambaye jina lake halikufahamika mara moja alikimbia
na bunduki na kisha kuelekea kusikojulikana.
Mkuu wa wilaya ya Karagwe ambaye pia ni mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo Bi. Darry Rwegasira akizungumza na
majira kwa njia ya simu alithibitisha kuuawa kwa askari hao.
Alisema katika eneo la tukio wameshuhudia damu zikiwa
zimetapakaa sehemu mbalimbali ikiwemo gari
waliokuwa nalo kuteketezwa kwa moto.
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya wilaya ya
Karagwe Nyakahanga Dkt. Andrew Cesari alithibitisha kupokea
miili ya marehemu hao.
Dkt. Cesari alisema uchunguzi wa kitabibu umebaini kuwa
vifo vya askari hao vilitokana na kipigo kikali kilichosababisha majeraha
katika sehemu mbalimbali za mwili, kuvuja damu nyingi na kisha kupelekea mauti
hayo.
Tukio
la jana la kuuawa kwa askari hao linafanya askari waliouawa na wananchi katika
mkoa wa Kagera katika kisichoazidi mwezi mmoja kufikia idadi ya askari wanne,
ambapo mwishoni mwa mwaka jana askari wawili waliuawa na wananchi wilayani
Ngara
Mwisho
No comments:
Post a Comment