Picha ya wageni waalikwa na waandishi wa habari wakicheza muziki kwa pamoja. |
Hawa nao wanafurahi kwa pamoja huku wakitafakari juu ya wajibu wao katika kuhabarisha na kuelimisha jamii |
Ni baadhi ya wadau wa habari na wageni waalikwa wakifuatilia sherehe hizo. |
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za uhuru wa vyombo vya habari akiongaza wageni waalikwa na waandishi wa habari mkoa wa Kagera . |
Na
Mwandishi maalum
Bukoba
MKUU
wa mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe amevitaka vyombo vya habari
mkoani humo kuacha kuendesha vipindi vinavyochochea ngono na badala yake
viandae na kutangaza au kuchapicha habari zenye kuleta tija kwa jamii.
Aidha
aliahidi kutoa shilingi milioni moja kwa klabu ya waandishi wa habari mkoani
humo, ikiwa ni mchango wake kuiwezesha kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa
ofisi za chama.
Bw.
Massawe alitoa wito huo jana wakati akifungua rasmi sherehe za uhuru wa vyombo
vya habari zilizofanyika katika manispaa ya Bukoba, na kuwakutanisha wanahabari
na wadau wa habari.
Alisema
kuwa baadhi ya radio za kijamii zilizopo mkoani hapa zinakalia kupiga nyimbo za
mapenzi badala ya kuandaa vipindi vya kuchochea maendeleo , jambo ambalo alidai
linachangia kuhamasisha jamii kufanya ngono zembe.
Bw.Massawe takwimu za kitaalum kwa sasa zinaonyesha
kwamba wananchi mkoani Kagera wamejisahau na kujikuta kiwango cha maambuzi ya
ukimwi kinapanda ghafla kutoka asilimia 3.4 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 9
mpaka sasa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment