Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Saturday, June 29, 2013

MGOGORO WA ARDHI MULEBA

Wanafunzi wa shule ya msingi iliyopo kata ya Mafumbo wakitoka mtoni kuchota maji ukosefu na huduma muhimu shuleni unasababisha kuvurugwa kwa ratiba za masomo .


Ofisi ya kata imefurika watu ingawa hata hawa wanataka kuingia lakini hakuna nafasi.

Hapa wananchi wanabadilishana mawazo kabla ya kufikia muafaka wa mgogoro huo, ambapo wafugaji na wakulima hao walikubaliana kuunda kamati ya kuchunguza ardhi inayodaiwa kuuzwa kinyume cha sheria.

BIASHARA YA NANASI

Karibu nanasi hapa ni eneo la Kyema Bukoba vijijni wauza nanasi wamesubiri wateja ambao wanaopita barabarani.

Ingawa upatikanaji wa nanasi hapa ni mkubwa lakini soko lake ni kidogo, ambapo nanasi hizo na matunda mengine yanaharibika kutokana na kukosa wateja. 

Wednesday, June 5, 2013

SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI


Wanafunzi wa shule ya msingi Tumaini iliyopo manispaa ya Bukoba wakifanya usafi katika maeneo yanayozunguka shule hiyo kwa lengo la kuweka mazingira ya safi, ambapo leo ni siku ya mazingira duniani.


Wanafunzi wa shule ya msingi Tumaini iliyopo manispaa ya Bukoba wakifanya usafi ikiwa ni siku ya mazingira duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 5 ikiwa na kauli mbiu mbalimbali.





Tuesday, June 4, 2013

ASKOFU KILAINI AIPONGEZA RASMU YA KATIBA

Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba Dkt. Methodius Kilaini akitoa ufafanuzi juu ya rasmu ya awali ya katiba ambayo ilitolewa jana na tume ya mabadiliko ya katiba, ambapo pamoja na mambo mengine amesema tume hiyo inatakiwa kupongezwa kutokana na udhubutu wake wa kuweka hadharani vitu vipya
Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba Dkt. Methodius Kilaini akisisitiza jambo juu ya rasmu ya katiba, ambapo ameipongeza rasmu hiyo kwani inaonyesha mwelekeo ya kuimarisha demokrasia.

Friday, May 31, 2013

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA??????

Zaidi ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bado kuna watu ambao wakipoteza wapendwa wao hulazimika kuwabeba kwenye machera hii ni kutokana na umasikini hususani maeneo ya vijijini, hali imepelekea kuwepo kwa makundi mawili yalionacho na wasiokuwa nacho.picha kwa hisani ya mtandao.

Thursday, May 30, 2013

KAMBI YA WANAFUNZI WA MICHEZO BUKOBA YAFUNGWA RASMI


anafunzi wa shule za msingi kutoka tarafa nne za Katerero, Bugabo, Rubare na Kyamutwara wakifurahia jambo wakati wa kufunga wa hafla fupi ya kufunga kambi ya michezo UMISHUMITA kambi hiyo wa siku tatu ilikuwa katika shule ya sekondari ya Maruku.



Wanafunzi wakiwa katika pozi wakisubiri kufungwa kwa kambi ya siku tatu ya  michezo.

Wanafunzi wa shule za msingi kutoka tarafa nne za Katerero, Bugabo, Rubare na Kyamutwara wakifuatilia maelekezo kutoka kwa walimu wao wa michezo katika kambi ya shule ya sekondari Maruku.

Wanafunzi wa shule za msingi kutoka tarafa nne za Katerero, Bugabo, Rubare na Kyamutwara wakifanya mazoezi kabla ya kufungwa kwa kambi ya michezo UMISHUMITA kambi hiyo wa siku tatu ilikuwa katika shule ya sekondari ya Maruku.
Mratibu wa kambi ya michezo ya wanafunzi wa shule za msingi akisoma majina ya wanafunzi 80 ambao wamechaguliwa kuwakilisha halmashauri ya wilaya ya Bukoba kwenye mashindano wa UMISHUMITA ngazi ya mkoa mashindano yanayotarajiwa kufanyika wilayani Muleba.

Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Bw. Clement Ndyamukama akifunga kambi hiyo ambayo imedumu kwa siku tatu na kushirikisha jumla ya wanafunzi 183 kutoka tarafa nne za halmshauri ya wilaya ya Bukoba.

Baadhi ya walimu waliokuwa wanafundisha kambi hiyo.


Tuesday, May 28, 2013

USAFIRI WETUUUU..............



Usafiri unaotumiwa na wananchi wengi wa mkoa wa Kagera (pikipiki ) zikiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoa wa Kagera.
 


Kwetu sisi hapa mjini Bukoba huu ndio usafiri wetu kutoka sehemu moja hadi nyingine.