Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Monday, August 6, 2012

MADEREVA KAGERA WAOMBA MAFUNZO YA MUDA MFUPI

Wahitimu hawa wanasoma risala kwa mgeni rasmi huku wakieleza a mambo yaliyofundishwa ambayo baadhi yake ni pamoja na polisi jamii, alama za barabarani, ukaguzi wa vyombo vya moto na uzimaji wa moto.
Livinus Feruzi Bukoba


WAENDESHA pikipiki katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba wameliomba jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera kuweka utaratibu wa kufanya mafunzo ya muda mfupi kuwa ya lazima kwa kila dereva ili kupunguza ajali za mara kwa mara.

 Madereva hao kutoka tarafa ya Bugabo Bukoba vijijini walitoa ombi hilo wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo maalumu ya muda mfupi, ambayo yalishirikisha waendesha pikipiki maarufu kwa jina la (bodaboda) wapatoa 84.

 Mafunzo hayo ya wiki moja yaliandaliwa na Chuo cha Mafunzo ya udereva cha Lake Zone kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu kwa madereva juu ya mabadiliko ya sheria za usalama barabarani yanayotokea mara kwa mar

 Akisoma risala kwa niaba ya madereva wenzake Bw. Charles Evarist alisema zaidi ya asilimia 40 ya vijana wa bodaboda waliopo katika tarafa ya Bugabo wanafanya shughuli hiyo bila kuwa na elimu juu ya sheria za usalama barabarani, na hivyo kupelekea ajali nyingi kutokea.


Bw. Evarist alisema ili kupunguza ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na Bodaboda, jeshi la polisi linatakiwa kuweka utaratibu wa kuhakikisha kila dereva anahudhuria mafunzo ya muda mfupi kwa lazima na sio hiari kama ilivyo sasa.

 Aidha waliomba polisi kuendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo kwa madereva wa Bodaboda waliopo mkoa wa Kagera ili kuhakikisha kila dereva anafahamu sheria za barabarani ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya sheria za barabarani.

 “Mheshimiwa mgeni rasmi tunaomba mafunzo haya ya muda mfupi yawe ya lazima na sio hiari kama ilivyo sasa na pia yaendelee kutolewa kwa maeneo mengine ili kupunguza ajali” alisema Bw. Evarist

Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kagera Bw. Winston Kabantega aliwataka madereva hao kubadilika kutokana na mafunzo hayo ili waweze kuepukana na ajali zinazosababishwa na uzembe .

 Bw. Kabantega ambaye pia ni Mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya udereva cha lake zone alisema madereva aliwaomba madereva hao kutoa taarifa polisi juu ya madereva wenzao wanaovunja sheria za usalama barabarani Mwisho

No comments:

Post a Comment