Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Thursday, August 16, 2012

MKUU WA MKOA WA KAGERA NA FUTARI JANA JIONI

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akiongea na waumini wa dhehebu la kiisilamu aliowaandalia futari kwenye viwanja vya Ikulu ndogo iliyoko katika manispaa ya Bukoba, alikwa akiwaeleza waapuuze waislamu wachache wanaotaka kukwamisha zoezi la sensa ya watu na makazi, alikuwa akiwaambia kuwa mungu ni mmoja.

Waumini wa dini ya Kiislamu na wageni waalikwa wakila futari iliyoandaliwa na Massawe kwenye viwanja vya Ikulu ndogo ya Bukoba.

Askofu Buberwa wa kanisa la kiinjiri la kirutheri diosisi ya kaskazini Magharibi alikuwa ni miongoni wmwa wageni walioalikwa kushiriki kwenye futari iliyoandaliwa na mkuu wa mkoa, kulia kwake ni sheikh Haruna Kichwabuta.

Mmiliki wa Cable inayosambaza mawasiliano katika manispaa ya Bukoba, Mohamed akiagana na mkuu wa mkoa baada ya kula futari. picha kwa hisani audax mtiganzi

No comments:

Post a Comment