Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Wednesday, August 8, 2012

VIONGOZI WA DINI NA WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA BUKOBA




VIONGOZI wa dini katika manispaa ya Bukoba ameonyesha kufurahishwa na juhudi kubwa zinazofanywa na meya wa manispaa ya Bukoba za kuweka mipango ya kuhakikisha inawaletea wananchi maendeleo , huku wakiahidi kutoa ushirikano ili kuwezesha kufikiwa kwa lengo husika.


Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti katika mkutano wa wadau wa maendeleo uliowakutanisha viongozi hao wa kiroho kwa ajili ya kujadili mipango ya maendeleo ambayo imepangwa kutekelezwa, walisema historia ya mji wa Bukoba haiendani na historia ya Kagera.


Mmoja wa viongozi hao askofu msaidizi wa Kanisa Katoliki jimbo la Bukoba Dkt. Methodius Kilaini alisema kwa muda mrefu sasa maendeleo ya manispaa ya Bukoba yamekuwa yakiathiriwa na kile alichokiita ‘siasa mfuniko’.


Alisema kutokana na baadhi ya wanasiasa kufunika baadhi vitu ambavyo vilikuwa vikwazo vya maendeleo huku wao wakiondoka baada ya kupata nafasi.


Awali Meya wa manispaa ya Bukoba Dkt. Anatory Amani aliwaeleza viongozi hao wa dini kwamba manispaa hiyo kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo imepanga kutekeleza miradi mikubwa ambayo itasaidia kutengeneza ajira mpya kwa vijana zipatazo 2,000 ikiwemo kubadilisha sura ya mji wa Bukoba.

Baadhi ya miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni pamoja wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi lenye ghorofa tisa, ujenzi wa kituo kikubwa cha mabasi chenye hadhi ya kimataifa, ujenzi wa soko la kisasa yenye huduma muhimu, na maduka maalum (supermakert). Mwisho

No comments:

Post a Comment