Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Wednesday, December 12, 2012

MJI WA BUKOBA NDANI YA MABOMU YA MACHOZI

 Nyumba ya mmiliki ambaye jina limeifadhiwa anayetuhumiwa na wananchi kwa kujihusisha na masuala ya ushirikina iko eneo la kata kashai katika manispaa ya Bukoba.
 Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya nyumba ya mtuhumiwa wa kujihusisha na masuala ya uchawi.
Mpangaji wa shirika lisilo la kiserikali la TADEPA kihama kwenye nyumba ya mmiliki anayetuhumiwa kwa kijihusha masuala ya uchawi.
 Huyu anayehama sio mwingine ni aliyekuwa mpangaji katika nyumba hiyo ambaye mtumishi wa kampuni ya simu ya Zantel.
Kundi la watu likiwa limejikusanya nje ya nyumba ya mtuhumiwa huyo, hata hivyo lilitawanywa na jeshi la polisi lililolazimika kutumia mabomu ya machozi.

 
Na Livinus Feruzi
Bukoba

POLISI  mkoa wa Kagera  jana walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wa kata ya Kashai manispaa ya Bukoba waliojikusanya katika nyumba ya mwalimu mmoja wa shule ya msingi ya Kashai wakitaka kuichoma moto kwa kumtuhumu kuhusika na vitendo vya kishirikina.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Richard Ngole alimtaja mwalimu aliyetaka kuchomewa nyumba kuwa ni Benadetha Katabaro, na kuwa wananchi walitaka kuchoma nyumba yake baada ya kudaiwa kukutwa na watoto wawili wa dada yake aitwaye Benedictor Bukende.

mwisho 

No comments:

Post a Comment