Kaimu mkurugenzi mkuu
wa mamlaka hiyo Bw. Ahmad Kilima akizungumza wakati
wa mkutano wa kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya viwango vya juu vya nauli
za mabasi ya masafa marefu vilivyopendekezwa na wasafirishaji.
Na Mwandishi wetu
Bukoba
Wakitoa maoni juu ya
kupanda nauli baadhi ya wadau waliwashutumu wasafirishaji mkoa wa Kagera kukaidi kufuata nauli
zinazopangwa na SUMATRA, ambapo wanajipangia nauli wanazotaka wao, na kuongeza
kuwa hakuna ya wao kuomba kupandishiwa nauli kwani tayari walishajipandishia.
Bw. Idrissa Suleiman
alisema kigezo wa wasafishaji cha kuomba kupandishiwa nauli kwa sababu ya
kupanda kwa gharama za maisha sio sahihi kwani gharama za maisha zimepanda kwa
kila mwananchi na sio wasafarishaji tu.
Hata hivyo
alitahadharisha kwamba endapo SUMATRA watakubali kupandisha nauli kama walivyopendekeza wasafirishaji gharama za maisha
zitazidi kupanda zaidi kwani mahitaji ya msingi ya binadamu yanategemea
usafishaji.
|
No comments:
Post a Comment