Wakuu wa idara mbalimbali za manispaa ya Bukoba waliohudhuria mkutano baina ya mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba na waandishi wa habari
Baadhi ya waandishi wakifuatilia tamko la mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Khamis Kaputa kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa soko kuu la mjini Bukoba.
Na Livinus Feruzi
Bukoba
HALMASHAURI ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,imesema
ujenzi wa soko jipya la kisasa utaanza mara baada ya taratibu kukamilika,huku
ikisisitiza kuwa haijafikia hatua ya kutangaza zabuni ya ujenzi wa soko hilo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba
Khamis Kaputa amesema hayo weakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia agizo la kamati ya halmashauri ya kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoani Kagera ambalo liliitaka serikali kutoa taarifa sahihi juu ya miradi yote ya maendeleo inayotarajiwa kujengwa ili kuepukana
na kero kutoka kwa wananchi.
Kaputa amesema kuwa upembuzi hakinifu wa mradi wa ujenzi wa
ujenzi wa soko jipya,haujawafikisha katika hatua ya kutangaza zabuni na kueleza
kuwa iwapo mradi huo utatekelezwa, mapato yatapanda kutoka wastani wa milioni
168 hadi bilioni mbili kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment