Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Wednesday, April 25, 2012

AU yaonya Sudan na Sudan kusini juu ya mzozo unaoendelea kati ya nchi hizo


Na Mwandishi wetu
 
MUUNGANO  wa nchi za Afrika umezitaka Sudan na Sudan Kusini kutekeleza mkataba wa amani kwa muundo mpya wa umoja wa  ulaya (AU) ikiwamo viongozi wa nchi husika  kuacha kutoa matamshi yanayochochea uhasama  baina yao na kusambaza propaganda ambazo zinachochea mzozo huo.

Kamishna wa baraza la usalama wa AU, Ramtane Lamamra alisema muungano huo utachukua hatua zinazostahili iwapo mojawapo ya nchi hizo itashindwa kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa katika muda uliopangwa.

Wajumbe wa baraza la usalama la umoja huo walimaliza kikao chao cha dharura kuhusu utata huo kwa kutoa maagizo mazito na kukariri njia ya kufuatwa ili kudhibiti hali hiyo mara moja, ikiwemo kutaka  pande zote mbili ziondoe majeshi yao katika mipaka hiyo inayo zozaniwa na wasitisha  mashambulio .

Umoja huo pia umependekeza kuwa ujumbe maalum wa waangalizi wa mipaka pamoja na kikosi cha walinda amani cha umoja wa mataifa kitumwe katika maeneo hayo katika kipindi cha wiki moja ijayo.

Baraza hilo la usalama la Umoja wa Afrika pia limeamua kuunda kamati itakayo chunguza malalamishi kutoka pande zote mbili hizi na kubaini ukweli kamili kuhusu masuala wanayosema kuwa yanazua utata huo.

Mwenyekiti wa baraza hilo Balozi Susan Price kutoka Marekani, alisema kuwa hii ni hatua muhimu ya uongozi kutoka Afrika na kuwa baraza hilo halitasita kuchukulia serikali hizo hatua ikiwa zitapuuza maagizo hayo.

Mwisho


Soko lililoshambuliwa Sudan Kusini (kwa hisani ya mtandao( BBC )

No comments:

Post a Comment