Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Saturday, April 21, 2012

CHADEMA wapingana na uamuzi wa halmashauri sakata la viwanja

Na Mwandishi wetu 
Bukoba 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Bukoba mkoa wa Kagera kimetoa msimamo wa kutaka wananchi 800 waliolipia viwanja kwa miaka kumi iliyopita, kupatiwa viwanja vyao bila kuongeza fedha tofauti na ilivyotangazwa na halmashauri ya manispaa ya Bukoba.
 
Msimamo huo ulitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bukoba Bw. Victor Shelejei wakati akiwahutubia maelefu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kata ya Bilele, manispaa ya Bukoba na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya mkoa na kitaifa.
 
Hata hivyo mgogoro huo umeonekana kuchukua sura mpya baada ya kukamilika kwa mradi wa upimaji viwanja 5,000, ambapo manispaa imetangaza kwamba wananchi watatakiwa kuongeza fedha ili kupatiwa viwanja tofauti na walivyolipia awali vinginevyo watarudishiwa fedha zao.
 
Akizungumza katika mkutano huo Bw. Shelejei alisema uamuzi wa kutaka wananchi kuongeza fedha ili kupatiwa viwanja vyao na kurudishiwa fedha kwa watakaoshindwa sio sahihi na kuwa ni kinyume na makubaliano kati ya wananchi husika na halmashauri.
 
Alisema lazima wananchi wapewe viwanja vyao na sio vinginevyo, ambapo alisema haiwezekani wananchi kuadhibiwa kwa sababu ya uzembe wa halmashauri na kutishia kuishtaki manispaa.

             
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bukoba Bw. Victor Shelejei akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kata ya Bilele.








Baadhi ya wananchi na wafuasi wa CHADEMA wakifuatilia hutuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa  na viongozi kadhaa wa chama hicho katika mkutano wa hadhara, maelfu ya wakazi wa manispaa ya Bukoba walijitokeza kusikiliza sera za chama na msimamo wa suala mbalimbali yanayohusu maisha yao.
Diwani wa CHADEMA viti maalum Bi. Winifrida Mkono akitoleta ufafanuzi mambo kadhaa yanayoendelea katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.  

  Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa  CHADEMA taifa Bw. Wilifred Rwakatare na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera akikabidhi  kadi kwa vijana ambao wamejiunga na chama hicho.

No comments:

Post a Comment