Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Wednesday, April 25, 2012

Wakulima wa kahawa Kagera kulipwa fedha za nyongeza

Mwenyekiti wa bodi ya cha kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera KCU 1990 LTD Bw. John Binunshu akifungua mkutano mkuu wa mizani uliofanyika jana katika ukumbi wa Bukoba Coop mjini Bukoba.
Mkaguzi mkuu wa COASCO Mkoa wa Kagera Bw. Kidai Yusuph akiwasilisha mahesabu ya chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera KCU ambayo yamekaguliwa kwa msimu ya mwaka 2010/11.
  
  
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa mizani wa KCU wakifuatilia taarifa ya mahesabu ya ushirika wao yaliyokaguliwa kwa msimu wa 2010/11.  
Mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wakichangia masuala mbalimbali juu ya malipo ya nyongeza ya mwisho kwa wakulima.





CHAMA Kikuu cha Ushirika mkoa wa Kagera (KCU 1990 LTD) kimetangaza malipo ya nyongeza kwa wakulima wa zao la kahawa, ambao waliuza katika chama hicho kwa msimu wa mwaka 2010/11 kutokana na kupata faida ya zaidi ya shilingi milioni 837.9.

Meneja mkuu wa KCU mkoa wa Kagera Bw. Vedasto Ngaiza alitangaza nyongeza ya malipo hayo jana wakati wa mkutano mkuu wa mizania, uliofanyika katika manispaa ya Bukoba na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Kagera.  

Akitangaza nyongeza hiyo Bw. Ngaiza alisema mkulima wa kahawa aina ya Arabica maganda atalipwa nyongeza ya shilingi 53.19 kwa kilo moja na Robusta maganda atalipwa shilingi 38.52 kwa kilo moja.

Aidha alisema Arabica safi msimu huu imekuwa tofauti na aina nyingine ya kahawa kutokana kuwa na bei kubwa kwenye soko la kimataifa, ambapo watalipwa nyongeza ya shilingi 106.39 kwa kilo moja na shilingi 77 kwa kahawa ya Robusta safi.

Hata hivyo takwimu zinaonyesha kwamba faida ya msimu huu imepanda mara mbili kulinganisha iliyopatikana msimu uliopita 2009/10, ambapo faida ilikuwa shilingi milioni 357.


mwisho 

No comments:

Post a Comment