Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Saturday, May 12, 2012

MADEREVA MKOA WA KAGERA WATAKIWA KUJIHAMI WAKIWA BARABARANI

kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Vitus Mlolere na  mkurugenzi wa chuo cha udereva cha lake zone Bw. Winston Kabantega wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi.
Ni baadhi ya washiriki wa mafunzo ya muda mfupi ambao ni waendesha pikipiki na magari kutoka Kyebitembe na Kalambi katika wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera , ambao wamehitimu na kukabidhiwa vyeti mafunzo hayo yaliandaliwa na chuo cha mafunzo ya udereva cha lake zone kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
Mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya udereva cha lake zone, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usalama mkoa wa Kagera Bw. Winston Kabantega akifafanua masuala kadhaa ikiwemo madereva kufuata sheria za barabarani na kujenga tabia ya kujihami ili kuepusha ajali zisizo za lazima
Ni baadhi ya washiriki wa mafunzo ya muda mfupi wakifuatilia nasaha zilizokuwa zikitolewe na viongozi mbalimbali.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Vitus Mlolere akifunga rasmi mafunzo hayo ya siku tano kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Henry Salewi.
Ni PC Joseph akiongoza wahitimu wa mafunzo hayo kuapa mbele ya mgeni rasmi Kaimu kamanda wa polisi Bw. Vitus Mlolere kwamba watabadilika na kufuata sheria za barabarani hasa baada ya mafunzo hayo ili kupunguza ajali.
Wahitimu wa mafunzo hayo wakifurahi baada ya kukabidhiwa vyeti vya mafunzo ya muda mfupi, ambavyo vitawawezesha kupata lesini mpya katika mabadiliko ya leseni kwa ajili ya kuendeshea vyombo vyao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Vitus Mlolere akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika wilaya ya Muleba, kata ya Nshamba , kalambi na Kyebitembe.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Vitus Mlolere akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika wilaya ya Muleba, kata ya Nshamba , kalambi na Kyebitembe.

No comments:

Post a Comment