Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Monday, May 21, 2012

TAKUKURU WAKONGA NYOYO ZA WANAFUNZI WA SEKONDARI WAPATAO 280


Wanachama wa klabu za wapinga rushwa katika mkoa wa Kagera kutoka shule za sekondari 14 wakifuatilia mada kuhusu wajibu wa wanachama wa klabu za wapinga rushwa katika mapambano dhidi ya rushwa wakati wa tamasha lililoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU.
Baadhi ya wavulana kutoka shule za sekondari 14 wakikimbia na magunia katika mbio za mita 100 wakati wa tamasha la wanachama wa klabu za kupinga rushwa.
Ni Baadhi ya wasichana katika mbio za mita 100 ya kukimbia na magunia wakati wa tamasha la wanachama wa klabu za kupinga rushwa.
Ni Wasichana wakikimbiza kuku
Huyu naye anafurahi baada ya kufanikisha kumkamata kuku ambaye alikuwa akikimbizwa na baadhi ya wavulana kutoka baadhi ya shule za wilaya ya Bukoba,tamasha hilo lilifanyika katika shule ya sekondari ya Mugeza iliyopo manispaa  ya Bukoba.
Wavulana wakivuta kamba
Na hawa ni wasichana wakivuta kamba

Afisa uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka makao makuu jijini Dar-es-Salaam, Bw. William Hergard akitoa mada kuhusu wajibu wa wanachama wa klabu za wapinga rushwa katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Wavulana wakiwa katika mashindano ya mita 100 kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Mugeza, zaidi ya wanafunzi 280 kutoka shule 14 walishiriki tamasha hilo.
Wasichana wakishindana katika kukimbia mbio za mita 100

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Bi. Domina Mkama aliyekalia kiti kirefu katikati akifuatili  michezo mbalimbali wakati wa tamasha hilo.
Na Mwandishi wetu
Bukoba

WANAFUNZI wa klabu za wapinga rushwa nchini, wametakiwa kutojiingiza katika vitendo vya ukiukwaji wa maadili, ikiwemo vitendo vya wizi wa mitihani na rushwa ya ngono.

Kauli hiyo ilitolewa  na afisa uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka makao makuu jijini Dar-es-Salaam, Bw. William Hergard wakati akitoa mada juu ya  wajibu wa wanachama wa klabu za wapinga rushwa katika mapambano dhidi ya rushwa.

Bw. Hergard aliwataka wanaklabu hao kuwa jasiri kukemea vitendo vya rushwa vinavyojitokeza ndani na nje ya shule na kufikisha elimu ya rushwa kwa wanafunzi wenzao ikiwa ni pamoja na jamii inayowazunguka.
MWISHO.
        

No comments:

Post a Comment