Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Monday, May 7, 2012

Sherehe za siku ya vyombo vya habari mkoa wa Kagera

Picha ya wageni waalikwa na waandishi wa habari wakicheza muziki kwa pamoja.


Baadhi wa wanahabari mkoa wa Kagera wakifurahi kwa pamoja kwa kucheza muziki wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari .
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za uhuru wa vyombo vya habari akifungua rasmi sherehe hizo, ambazo pia zilihudhuriwa na wadau mbalimbali .kamanda wa Takukuru mkoa wa Kagera Bi Domina Mkama Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw. Samwel Kamote na kaimu kamanda wa polisi mkoa Bw. Vitus Mlolore .
Hawa nao wanafurahi kwa pamoja huku wakitafakari juu ya wajibu wao katika kuhabarisha na kuelimisha jamii
Ni baadhi ya wadau wa habari na wageni waalikwa wakifuatilia sherehe hizo.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika  sherehe za uhuru wa vyombo vya habari akiongaza wageni waalikwa na waandishi wa habari mkoa wa Kagera .

Na Mwandishi maalum
Bukoba

MKUU wa mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe amevitaka vyombo vya habari mkoani humo kuacha kuendesha vipindi vinavyochochea ngono na badala yake viandae na kutangaza au kuchapicha habari zenye kuleta tija kwa jamii.

Aidha aliahidi kutoa shilingi milioni moja kwa klabu ya waandishi wa habari mkoani humo, ikiwa ni mchango wake kuiwezesha kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za chama.

Bw. Massawe alitoa wito huo jana wakati akifungua rasmi sherehe za uhuru wa vyombo vya habari zilizofanyika katika manispaa ya Bukoba, na kuwakutanisha wanahabari na wadau wa habari.

Alisema kuwa baadhi ya radio za kijamii zilizopo mkoani hapa zinakalia kupiga nyimbo za mapenzi badala ya kuandaa vipindi vya kuchochea maendeleo , jambo ambalo alidai linachangia kuhamasisha jamii kufanya ngono zembe.

Bw.Massawe  takwimu za kitaalum kwa sasa zinaonyesha kwamba wananchi mkoani Kagera wamejisahau na kujikuta kiwango cha maambuzi ya ukimwi kinapanda ghafla kutoka asilimia 3.4 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 9 mpaka sasa.

Mwisho


No comments:

Post a Comment