Karibu WanaKagera ili tuunganishe nguvu zetu kwa pamoja katika harakati za kujenga Kagera yetu.
Saturday, October 13, 2012
KCU KAGERA WAMDANGANYA WAZIRI CHIIZA
waziri wa chakula, kilimo na ushirika Bw. Christopher Chiiza akizungumza na wajumbe wa bodi ya chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera KCU juu tuhuma za wizi ndani ya chama hicho
Mwenyekiti wa bodi ya KCU bw. John Binushu akisoma taarifa za chama hicho ingawa maelezo yake walikuwa taofauti na hali halisi na hivyo kwa wakulima na watu wengine wanaofahamu KCU
baadhi ya viongozi wa KCU wakimsikiliza waziri CHIIZA
Na mwandishi wetu. Bukoba
WAZIRI wa
kilimo chakula na ushirika Bw. Christopher Chiza amewatuhumu wakaguzi wa vyama
vya ushirika kuwa chanzo za kudhoofisha ushirika kwa kile alichodai wanapotumwa
kufanya ukaguzi wanakuja na taarifa nzuri licha ya kuwepo malalamiko ya
matumizi mabaya ya fedha.
Waziri Chiza
alitoa kauli hiyo mjini Bukoba wakati akizungumza na wajumbe wa bodi ya chama
kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera KCU 1990 LTD baada ya malalamiko na tuhuma
zilizoibuliwa hivi karibuni juu ya matumizi mabaya ya fedha.
Alisema
yanapotokea malalamiko kwenye vyama vya ushirika, wakaguzi wanatumwa kukagua
matumizi ili hatua za kisheria na kinidhamu ziweze kwa wahusika lakini
wanapokwenda kukagua wanaandaa taarifa nzuri zinaonyesha hakuna matumizi mabaya
ya fedha .
“Licha ya
kuwepo malalamiko mengi ya KCU kula fedha za wakulima wakaguzi kila wakienda
kukagua wanaleta taarifa nzuri na tayari zipo taarifa kwamba wanapotumwa
wanapewa fedha na kuandaa taarifa nzuri ambazo hazionyeshi kasoro” alisema
Waziri Chiza.
Kwa mujibu wa
waziri Chiza ushirika kwa sasa umedorola taofauti na ilivyokuwa miaka iliyopita
na kuwa ofisa yake ina mafaili mengi ambayo yanaonyesha KCU wanakula fedha za
wakulima.
Alisema
miongoni mwa sababu za kudorola kwa ushirika ni ukosefu wa uaminifu na viongozi
wanaochaguliwa kuongoza ushirika huo kupenda kujinufaisha wao badala ya
wakulima ambao ndio walengwa na wamiliki wakuu wa ushirika.
Awali akitoa
taarifa kwa waziri huyo Mwenyekiti wa bodi ya KCU Bw. John Binunshu alisema kwa
sasa KCU haina tatizo kwani wastani wa shilingi milioni 10 hutolewa kila chama
kila wiki kwa ajili ya malipo ya wakulim.
Hata hivyo
taarifa hiyo ilionekana kupingana na hali halisi ilivyo baada ya kudai kwamba
mkoani Kagera hakuna waganda wanaonunua kahawa kwa bei nzuri tofauti na KCU,
ambapo kauli hiyo inapingana na kauli ya baadhi ya wakulima wilayani Muleba
ambao hivi karibuni walikaririwa wakigoma kuiuzia KCU kahawa baada ya kushusha
bei.
No comments:
Post a Comment