Mwonekano wa sasa wa kanisa katoliki jimbo la Bukoba, humu ndipo marehemu kardinali Laurean Rugambwa atazika kama makao yake ya milele |
Na mwandishi wetu
Bukoba
BAADA ya maandalizi ya muda mrefu ya kuhamisha masalia
ya mwili wa aliyekuwa Kardinali wa kwanza Afrika, marehemu Laurean Rugambwa
kutoka katika kanisa la Kashozi alikozikwa kwa muda sasa masalia hayo yataamishwa
rasmi kesho, huku Waziri mkuu Bw. Mizengo Pinda akitarajiwa kuwasili kesho
mjini Bukoba ili kushiriki tukio hilo.
Kanisa kuu jimbo la katoliki ambalo lilikuwa
likikarabatiwa kwa muda mrefu sasa limeshuhudiwa likiwa katika maandalizi ya
mwisho, ambapo shamrashara za baadhi ya wakazi mjini Bukoba juu ya tukio hilo
zikiwa zimeanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa
mkoa wa Kagera na kusainiwa na Bw. Richard Kwitega kwa niaba ya katibu tawala
mkoa huo, inaonyesha kuwa Waziri Pinda atawasili saa 9.30 alasiri katika uwanja
wa ndege uliopo mjini Bukoba.
Bw. Kwitega alisema mbali na Bw. Pinda kushiriki
mazishi ya Kardinali Rugambwa jumapili wiki hii pia atashiriki katika
kutabaruku kanisa kuu la jimbo katoliki la Bukoba kabla ya kuondoka mjini
Bukoba saa 10 alasiri siku ya jumapili(7/10/2012).
-->
No comments:
Post a Comment