Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Friday, November 2, 2012

MCT YATANGAZA NEEMA KWA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA

Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga aliyesimama akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Kagera wakati wa mkutano uliofanyika mjini Bukoba.

Waandishi wa habari na wadau wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika manispaa ya Bukoba.
Na Livinus Feruzi
Bukoba

BARAZA la habari Tanzania (MCT) limesema kuanzia mwakani kuna  mpango wa kuanza kuendesha mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti habari katika mazingira hatarishi.

Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga alisema hayo jana mjini Bukoba wakati wa majumuisho ya mkutano baina ya wadau wa habari mkoa wa Kagera na waandishi wa habari.

Bw. Mukajanga alisema Tanzania inapoelekea, mazingira ya waandishi wa habari kutekeleza wajibu wao huenda yakawa magumu zaidi kutokana na matukio yanayotakiwa kufanyiwa coverage kama mikutano au mahubiri kugeuka kuwa sehemu za hatari.

Alisema waandishi watapatiwa mafunzo ili kuwawezesha kuelewa msingi ya jinsi ya kufanya kazi zao katika mazingira ya hatari na kuongeza kuwa hatarishi kwa waandishi wa habari yanazidi kuongezeka.

“Tunapokwenda Tanzania waandishi watazidi kuwa na mazingira magumu zaidi ya kutekeleza wajibu wao, maana kwa sasa mikutano au mahubiri ambayo lazima yafanyiwe coverage (yaripotiwe) yamekuwa ya hatari” alisema Bw. Mukajanga.


Mwisho
 

No comments:

Post a Comment