-->
Bukoba
BAADA ya kilio cha muda mrefu juu walemavu nchini kutopewa fursa za
kisiasa, kiuchumi na majengo ya umma kujengwa bila kuzingatia mahitaji
ya kundi hilo, kilio hicho huenda kikapatiwa ufumbuzi baada ya
serikali kuziagiza taasisi zake kuimarisha fursa hizo ili kuwapunguzia
matatizo.
Mara kadhaa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania
(SHIVYAWATA) mkoa wa Kagera limekuwa likilalamikia walemavu kunyimwa
fursa kulinganisha na watu wasio na ulemavu, huku miundombinu na
majengo ya umma yakijengwa bila kuzingatia mahitaji yao.
Afisa maendeleo na ustawi wa jamii mkoa wa Kagera Bi. Rebecca Gwambasa
alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini Bukoba wakati akifungua mafunzo
ya siku nne juu ya sheria ya ajira ya mwaka 2004 na sheria ya walemavu
mwaka 2010 kuhusu mahusiano kazini, ambapo yalishirikisha walemavu 50
kutoka wilaya ya Muleba na Missenyi.
Kwa mujibu wa Bi. Gwambasa serikali kupitia Ofisi ya Waziri mkuu wa
tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI )tayari imeziagiza
idara zote za serikali na mamlaka husika kupanua na kuimarisha fursa
za kisiasa, kiuchumi ikiwa ni pamoja na ajira kwa walemavu.
Kuhusu miundombinu alisema TAMISEMI imeagiza kuhakikisha kwamba ujenzi
wa majengo yanayotoa huduma za umma yanajengwa kwa kuzingatia mahitaji
ya raia wote bila kujali maumbile yao.
Aidha alisema wameagizwa kubaini walemavu wanaoweza kufanya kazi za
uzalishaji na maeneo wanakoishi ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa
ikiwa ni hatua ya utekeleza sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka
2010.
“Serikali kwa upande wake inatambua umuhimu na mchango wa jamii ya
watu wenye ulemavu katika harakati za maendeleo na ndio maana
ilichukua hatua ya kuifanyia marekebisho sheria ya namba mbili na
tatu” alisema Bi. Gwambasa.
Aliwahakikishia walemavu kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao ili
kuwezesha kutimizwa kwa haki zao ikiwemo kutafuta ufumbuzi kwa baadhi
ya matatizo yanayowakabili walemavu.
“Siku zote serikali itahakikisha kwamba sheria ya watu wenye ulemavu
ya mwaka 2010 inatekelezwa na makundi yote ambayo ni serikali kuu,
halmashauri, mashirika binafsi na wananchi kwa ujumla ili kuleta
ufanisi” aliongeza afisa huyo.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera
Rebeca Gwambasa akifungua semina
-->Na
Livinus FeruziBukoba

No comments:
Post a Comment