Baadhi ya wajumbe wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya |
Na Mwandishi wetu
Bukoba
SHIRIKISHO
la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) mkoa wa Kagera limeitaka
tume ya mabadiliko ya katiba mpya kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwa
walemavu wakati wa mikutano ya kutoa maoni juu ya uundwaji wa katiba mpya ili
katiba itakayopatika iwe ya Watanzania wote.
Kauli
ya shirikisho hilo imekuja wiki chache baada ya tume ya mabadiliko ya katiba
mpya kuhitimisha zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wananchi katika mkoa wa
Kagera, ambapo changamoto kubwa ilionekana kuwa ni makundi mengi ya walemavu
kushindwa kutoa maoni yao kutokana na kukosa mawasiliano.
Mwenyekiti
wa SHIVYAWATA mkoa wa Kagera Bw. Suleiman Idrissa alisema hayo leo (jana) mjini
Bukoba wakati wa semina ya siku nne kwa watu wenye ulemavu kutoka wilaya ya
Muleba na Missenyi juu ya sheria ya ajira ya mwaka 2004 na sheria ya walemavu
mwaka 2010 kuhusu mahusiano kazi ni.
Bw.
Idrissa alisema tathimini iliyofanywa na shirikisho hilo baada ya tume kumaliza
zoezi hilo mkoani hapa imebaini kuwa asilimia kubwa ya walemavu hasa wasioona,
wasiosikia na viziwi hawakufanikiwa kutoa maoni yao licha ya kujiandaa siku
nyingi kwa ajili ya zoezi hilo.
Alisema
hata baadhi ya walemavu waliofika kwenye mikutano ya kukusanyia walishindwa
kufikisha maoni yao kwa tume husika baada ya kukosa mawasiliano baina yao,
maandishi wa nukta kwa watu wasioona na watu wa kutafsiri lugha za ishara .
Hata
hivyo shirikisho hilo limesema kwa mapungufu yaliyojitokeza tayari wameingiwa
na wasiwasi kama katiba itakayopatikana itakidhi matakwa ya walemavu kutokana
kile alichodai kwamba walemavu ndio waathirika wakubwa wa katiba iliyopo.
No comments:
Post a Comment