Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Tuesday, September 11, 2012

WAANDISHI WA HABARI KAGERA WAUNGANA NA WENZAO KUPINGA MAUAJI YA Mwangosi

Wanahabari wakimsikiliza Mwenyekiti wa klabu wa waandishi kagera baada ya kupokea maandamano ya amani ya kupinga mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa channel ten Daudi Mwangosi

Askari wa usalama barabarani akiongoza maandamo ya waandishi wa habari mkoa wa Kagera

Na mwandishi wetu
Bukoba
WAANDISHI wa habari mkoa wa Kagera wameungana na waandishi wenzao  nchini kufanya maandamano ya amani ya kulaani mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha television cha Channel Ten marehemu Daud Mwangosi aliyeuawa wakati akitekeleza wajibu wake.

Maandamano hayo ya amani ambayo yalipita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bukoba, ambapo waandishi wa habari walibeba mabango kadhaa ya yaliyokuwa na ujumbe wa kulaani mauaji ya Mwangosi pamoja na raia wengine waliopoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

Maandamano hayo yaliyoanzia eneo la stendi kuu wa Bukoba yalipokelewa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kagera (KPC) Bw. John Rwekanika katika ofisi za chama hicho.

Akisoma hotuba fupi baada ya kupokea maandamano hayo Bw. Rwekanika alisema wanahabari mkoa wa Kagera hawaridhishwi na matumizi ya nguvu kubwa zinazotumiwa na jeshi la polisi katika kuzima maandamano na kisha kupelekea vifo vya raia wasiona hatia yakiwemo mauaji ya Daud Mwangosi.

Alisema mauaji ya Mwangosi yamepelekea jeshi la polisi kuingia katika uhusiano wenye shaka baina yao na waandishi wa habari hasa kutokana na ushahidi wa picha za tukio hilo kuonyesha mauaji hayo ya kikatili, kinyama na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kutokana na mauaji hayo KPC mkoa wa Kagera wametoa tamko la kutaka askari wanaohusishwa na kifo hicho kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi unaondelea ufanyike kwa uhuru na haki, ikiwemo kuwajibishwa kwa Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda.

“Kwa kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alikuwepo katika tukio hilo na alikataa kutoa msaada wa kuokoa maisha ya Mwangosi wakati askari wake wakimsurubu tunamtaka awajibike au au kuwajibishwa” alisema Rwekanika kwa niaba ya wanahabari mkoa wa Kagera.

Alisema iwapo mwenendo wa suala hilo hautaleta tija na kutoridhishwa na majibu ya kamati iliyoundwa na waziri wa mambo ya ndani watashirikiana na asasi nyingine za kutetea haki za binadamu watatafuta njia bora ya kuishitaki serikali.

Mwisho

No comments:

Post a Comment