Na Mwandishi wetu
MUUNGANO wa nchi za Afrika
umezitaka Sudan na Sudan Kusini kutekeleza mkataba wa amani kwa muundo mpya wa umoja
wa ulaya (AU) ikiwamo viongozi wa nchi husika
kuacha kutoa matamshi yanayochochea
uhasama baina yao na kusambaza
propaganda ambazo zinachochea mzozo huo.
Kamishna wa baraza la usalama wa AU, Ramtane Lamamra alisema
muungano huo utachukua hatua zinazostahili iwapo mojawapo ya nchi hizo
itashindwa kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa katika muda uliopangwa.
Wajumbe wa baraza la usalama la umoja huo walimaliza kikao
chao cha dharura kuhusu utata huo kwa kutoa maagizo mazito na kukariri njia ya
kufuatwa ili kudhibiti hali hiyo mara moja, ikiwemo kutaka pande zote mbili ziondoe majeshi yao katika
mipaka hiyo inayo zozaniwa na wasitisha
mashambulio .
Umoja huo pia umependekeza kuwa ujumbe maalum wa waangalizi
wa mipaka pamoja na kikosi cha walinda amani cha umoja wa mataifa kitumwe
katika maeneo hayo katika kipindi cha wiki moja ijayo.
Baraza hilo la usalama la Umoja wa Afrika pia limeamua
kuunda kamati itakayo chunguza malalamishi kutoka pande zote mbili hizi na
kubaini ukweli kamili kuhusu masuala wanayosema kuwa yanazua utata huo.
Mwenyekiti wa baraza hilo Balozi Susan Price kutoka
Marekani, alisema kuwa hii ni hatua muhimu ya uongozi kutoka Afrika na kuwa
baraza hilo halitasita kuchukulia serikali hizo hatua ikiwa zitapuuza maagizo
hayo.
Mwisho
Soko
lililoshambuliwa Sudan Kusini (kwa hisani ya mtandao( BBC )
No comments:
Post a Comment