Mwenyekiti wa bodi ya cha kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera KCU 1990 LTD Bw. John Binunshu akifungua mkutano mkuu wa mizani uliofanyika jana katika ukumbi wa Bukoba Coop mjini Bukoba. |
Mkaguzi mkuu wa COASCO Mkoa wa Kagera Bw. Kidai Yusuph akiwasilisha mahesabu ya chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera KCU ambayo yamekaguliwa kwa msimu ya mwaka 2010/11. |
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa mizani wa KCU wakifuatilia taarifa ya mahesabu ya ushirika wao yaliyokaguliwa kwa msimu wa 2010/11. |
CHAMA Kikuu
cha Ushirika mkoa wa Kagera (KCU 1990 LTD) kimetangaza malipo ya nyongeza kwa
wakulima wa zao la kahawa, ambao waliuza katika chama hicho kwa msimu wa mwaka
2010/11 kutokana na kupata faida ya zaidi ya shilingi milioni 837.9.
Meneja mkuu
wa KCU mkoa wa Kagera Bw. Vedasto Ngaiza alitangaza nyongeza ya malipo hayo
jana wakati wa mkutano mkuu wa mizania, uliofanyika katika manispaa ya Bukoba
na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Kagera.
Akitangaza
nyongeza hiyo Bw. Ngaiza alisema mkulima wa kahawa aina ya Arabica maganda
atalipwa nyongeza ya shilingi 53.19 kwa kilo moja na Robusta maganda atalipwa
shilingi 38.52 kwa kilo moja.
Aidha alisema
Arabica safi msimu huu imekuwa tofauti na aina nyingine ya kahawa kutokana kuwa
na bei kubwa kwenye soko la kimataifa, ambapo watalipwa nyongeza ya shilingi
106.39 kwa kilo moja na shilingi 77 kwa kahawa ya Robusta safi.
Hata hivyo takwimu zinaonyesha kwamba faida ya msimu huu imepanda mara mbili
kulinganisha iliyopatikana msimu uliopita 2009/10, ambapo faida ilikuwa
shilingi milioni 357.
mwisho
No comments:
Post a Comment