Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Saturday, April 28, 2012

Wamachinga Bukoba waitisha kugoma kuhamia machinjioni

Ni baadhi ya wafanyabiashara maarufu kama machinga ambao wanatakiwa kuhama kutoka eneo la kandokando mwa barabara ya Uganda kwenda eneo la Machinjioni.

Na Mwandishi wetu 
Bukoba 

WAFANYABIASHARA wadogo maarufu kama wamachinga wanaopanga bidhaa zao kandokando mwa barabara ya Uganda eneo la Nyumba ya Vijana, wameitaka manispaa ya Bukoba kuweka miundombinu inayoridhisha katika eneo jipya inakotaka kuwahamishia kabla ya kutekeleza zoezi hilo.

Wamachinga hao walisema kuwa walipokutana na uongozi wa manispaa hiyo mwaka jana waliainisha baadhi ya masuala yanayotakiwa kuwepo katika eneo hilo ndipo waweze kuhamia, ikiwa ni pamoja na kuwajenge vyoo kwenye maeneo hayo mapya, kuweke mfumo wa maji na stoo kwa ajili ya kutunzia bidhaa.

Mmoja wa wafanyabiashara hao Bw. George Laurian alisema kuwa mwaka 2008 walikwenda katika eneo hilo na kupewa maeneo ya kujenga vibanda lakini ghafla walijitokeza watu na kuwafukuza wakidai ni maeneo yao, hali iliyosababisha warejee katika maeneo yao ya siku zote.

“Wasitufanye kama wakimbizi katika nchi yetu, tumechukua mikopo ambayo tunatakiwa kurejesha, watuandalie mazingira yanayoridhisha sisi tuko tayari kuhama hapa, wateja wetu wakijua tuko huko watatufuata” alisema mfanyabiashara huyo.

Akizungumzia suala hilo meya wa manispaa ya Bukoba Dkt. Anathory Amani alisema mchakato wa kuwahamishia wamachinga katika eneo la Machinjioni uko hatua za mwisho, na kuwa kufikia wiki ijayo utekelezaji wake utaanza.


Mwisho.

No comments:

Post a Comment