Na Mwandishi wetu
Bukoba
CHAMA cha Demokrasia
na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Bukoba mkoa wa Kagera kimetoa msimamo wa kutaka
wananchi 800 waliolipia viwanja kwa miaka kumi iliyopita, kupatiwa viwanja vyao
bila kuongeza fedha tofauti na ilivyotangazwa na halmashauri ya manispaa
ya Bukoba.
Msimamo huo ulitolewa
na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bukoba Bw. Victor Shelejei wakati akiwahutubia
maelefu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kata ya
Bilele, manispaa ya Bukoba na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho
ngazi ya mkoa na kitaifa.
Hata hivyo mgogoro
huo umeonekana kuchukua sura mpya baada ya kukamilika kwa mradi wa upimaji
viwanja 5,000, ambapo manispaa imetangaza kwamba wananchi watatakiwa kuongeza
fedha ili kupatiwa viwanja tofauti na walivyolipia awali vinginevyo
watarudishiwa fedha zao.
Akizungumza katika
mkutano huo Bw. Shelejei alisema uamuzi wa kutaka wananchi kuongeza fedha ili
kupatiwa viwanja vyao na kurudishiwa fedha kwa watakaoshindwa sio sahihi na
kuwa ni kinyume na makubaliano kati ya wananchi husika na halmashauri.
Alisema lazima wananchi
wapewe viwanja vyao na sio vinginevyo, ambapo alisema haiwezekani wananchi kuadhibiwa kwa sababu ya uzembe wa halmashauri na kutishia kuishtaki manispaa.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bukoba Bw. Victor Shelejei akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kata ya Bilele. |
Diwani wa CHADEMA viti maalum Bi. Winifrida Mkono akitoleta ufafanuzi mambo kadhaa yanayoendelea katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba. |
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CHADEMA taifa Bw. Wilifred Rwakatare na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera akikabidhi kadi kwa vijana ambao wamejiunga na chama hicho.
No comments:
Post a Comment