Baadhi ya madereva wa magari na pikipiki wakifuatilia maelezo jinsi ya kukabiliana na ajali za barabarani wakati wa mafunzo ya muda mfupi.
Na mwandishi wetu
Muleba
MADEREVA wa magari na pikipiki mkoa wa Kagera wameshauriwa
kuacha tabia ya kuwaona askari wa usalama barabarani kama ‘wanonko’ kutokana na kuwakamata na kuwawajibisha
wanaokwenda kinyume na badala yake watambue kwamba wanalenga kuokoa maisha yao.
Mkuu mpya wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa
Kagera Bw. William Mkonde alitoa wito huo jana katika kata ya Kamachumu wilayani
Muleba wakati akifungua mafunzo ya waendesha pikipiki na magari ikiwa ni mara
yake ya kwanza kukutana wadereva tangu
alipohamia mkoani hapa.
Bw. Mkonde alisema madereva wengi wanachukulia askari
wa kikosi cha usalama barabarani kama ‘wanonko’ kutokana na juhudi za kikosi
hicho za kuwakamata na kuwajibishwa hasa kwa kukiuka sheria na kanuni za
usalama na kuwa juhudi hizo zinalenga kuokoa maisha yao.
Alisema madhara ya ajali za barabarani ni makubwa na
kuongeza kuwa mbali na madereva kuonekana waathirika wakubwa pia jamii taifa kwa ujumla wanaathirika hasa pale raia
wanapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu.
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa
Kagera Bw. Winston Kabantega alionya madereva kuancha ya dhana ambayo kwa muda
mrefu imejengeka miongoni mwao kwamba wanaweza kupata leseni mpya za kuendeshea
vyombo hivyo bila ya vigezo vilivyotangazwa na serikali.
Bw. Kabantega ambaye pia ni Mkurugenzi wa chuo cha
mafunzo ya udereva cha lake zone alisema madereva wengi bado wanafikili kwamba
wanaweza kulipa fedha bila ya vigezo na kisha kupatiwa leseni, jambo ambalo
alisema kwa sasa haliwezekani.
Mafunzo hayo ya muda mfupi yanatolewa na chuo cha
Udereva cha lake zone kwa kushirikana na jeshi la polisi kikosi cha usalama
barabarani ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa jeshi hilo kutoa elimu kwa
madereva mkoani haoa ili kupunguza ajali za mara kwa mara.
Mwisho
|
No comments:
Post a Comment