Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Thursday, June 28, 2012

TANNA KAGERA YAPATA SAFU MPYA YA VIONGOZIIIIIIIII..

 
Muuguzi mkuu wa mkoa wa Kagera Christine Ntangeki ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi akitoa wito kwa viongozi hao waliochaguliwa

Wajumbe wakifuatilia mkutano wa uchaguzi
Mwenyekiti mpya wa TANNA akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumchagua kushika nafasi hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kuhakikisha anafuatilia kero za wauguzi mkoa wa Kagera ili serikali kupitia wizara husika iweze kuzipatia ufumbuzi.
Katika ni mwenyekiti wa TANNA tawi la mkoa wa Kagera,  ambaye amemaliza  muda wake Bw. Deusdedith Rweyemamu akifuatilia matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yakitangazwa na msimamizi wa uchaguzi.
Safu mpya ya uongozi wa chama cha wauguzi Tanzania tawi la mkoa wa Kagera wakiwa meza kuu baada ya kuchaguliwa  wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi.
Na Livinus Feruzi
Bukoba

CHAMA cha wauguzi Tanzania tawi la mkoa wa Kagera kimepata safu mpya ya uongozi  baada ya waliokuwepo kumaliza muda wao ambapo Pius Rugakingira amechaguliwa kuwa Mwenyekiti chama hicho huku Paul Matondane akichaguliwa msaidizi wake.

Aidha Evania Fyita alichaguliwa kuwa katibu chama hicho na Gelaid Kabyemela alichaguliwa kuwa katibu msaidizi, huku Bi. Sofia Musoke ambaye alikuwa Mweka hazina katika kipindi kilichopita ameendelea kushika nafasi hiyo.

Katika uchaguzi huo ulifanyika jana muuguzi mkuu wa mkoa wa Kagera Bi. Christine Ntangeki aliwataka wauguzi mkoa wa Kagera kuhakikisha wanakata leseni za uuguzi ili waweze kutambuliwa na kukudhi mahitaji ya kisheria ikiwemo kuepukana na matatizo ambayo wanaweza kukumbana nayo.

Aliwataka viongozi wa TANNA katika matawi mbalimbali ya mkoa wa Kagera kuwaandikia barua wauguzi ambao hawana leseni za kuwakumbusha umuhimu na wajibu wao wa kukata leseni ili waweze kuepukana madhara wanayoweza kukumbana nayo.

Mwisho

No comments:

Post a Comment