Wananchi wa jimbo la Bukoba wakimpokea mbunge wa jimbo hilo ambaye pia Waziri wa maliasili na utalii alipowasili katika uwanja wa uhuru kwa ajili ya mkutano wa hadhara |
Na Mwandishi wetu
Bukoba
WAZIRI wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki
ameridhia uamuzi wa kuvunja soko kuu la Bukoba na kulijenga upya ili kulifanya
liwe la kisasa huku akiwahakikishia wafanyabiashara katika soko hilo kwamba halitavunjwa
mpaka lipatikane eneo mbadala la kufanyia biashara zao.
Balozi Kagasheki ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la
Bukoba mjini alisema hayo mjini Bukoba katika mkutano wa hadhara, uliofanyika
mwishoni mwa wiki kwenye uwanja uhuru, ambapo mkutano huo pamoja na mambo
mengine ulilenga kuwashukuru wapiga kura wake.
Alisema suala la kuvunja soko ambalo linapingwa na wafanyabiashara
na kisha kupelekea kuwepo kwa mgogoro baina yao na halmashauri ya manispaa ya Bukoba kwa
sasa halina nafasi na kusisitiza kuwa lazima livunjwe ili lijengwa upya.
Waziri Kagasheki alisema soko la mjini Bukoba
limekuwepo tangu zamani na kuwa miji mingi hapa nchini wamebadili masoko na
kujenga ya kisasa isipokuwa Bukoba na
kuongeza kuwa ni lazima hata Bukoba ibadilike ili kwenda na wakati.
MWISHO
No comments:
Post a Comment