Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Monday, June 11, 2012

POLISI KAGERA WAUA JAMBAZI NA KUNASA SILAHA ZA KIVITA


Na Mwandishi wetu
Bukoba 
 
JESHI la polisi mkoa wa Kagera limefanikiwa kukamata bunduki tatu, risasi 246, mabumu matatu ya kurushwa kwa mkono, magazine saba na sare mbili zinazofanana kabisa na za Jeshi la wananchi Tanzania baada ya kudaiwa kumuua mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi, wakati wa harakati za kutaka kuvamia mgodi wa Barrick wa Tulawaka uliopo wilayani Biharamulo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Philip Kalangi aliwaambia waandishi wa habari kuwa silaha hizo zilikamatwa mwishoni mwa wiki katika eneo la Mavota wilaya ya Biharamulo baada ya shambulizi la kurushiana risasi kati ya askari polisi na mtu anayesadikiwa kuwa jambazi.


Bw. Kalangi alisema polisi walipata taarifa za siri kutoka kwa raia wema kwamba majambazi wanataka kuvamia mgodi wa dhahabu wa Tulawaka, ambapo polisi chini ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Bw. Peter  Matagi waliweka mtego na hivyo kufanikiwa kuzima tukio hilo la ujambazi.


Alitaja aina ya silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na bunduki mbili aina ya AK47 na SMG moja, ambapo mbili zilikuwa zimefungwa kwenye mfuko wa kiroba, huku moja akiitumia kujaribu kujihami, ambayo inaelezwa haikumsaidia.


Bunduki hizo zilikuwa na namba UC- 55231990 na UC-16081998 na moja ya SMG yenye namba 56128033262.

Mbali na silahi hizo pia polisi walifanikiwa kukamata viatu pea moja vya kijeshi na makoti mawili ya kujifuniki mvua, na kuwa mwili wa jambazi huyo ambaye mpaka sasa bado hajatambuliwa umehifadhiwa katika hospitali teule ya wilaya Biharamulo.

mwisho 

No comments:

Post a Comment