Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Tuesday, June 26, 2012

POLISI KAGERA WANASA VIFAA MBALIMBALI VYA WIZI

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Philip Kalangi akionyesha bunduki ambayo ilikamatwa na mfuko wa bangi iliyokamatwa wakati wa operashem maalum pembeni mwake ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Kagera Bw. Peter Matagi.vifaa ambavyo vimekamatwa

Ni baadhi ya vifaa vya maabara ambavyo vimekamatwa kwa mwalimu Alfred Sitayo akivitumia katika kufundishia masomo ya ziada


Bukoba

JESHI la polisi mkoa wa Kagera limefanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vinavyosadikiwa kuwa vya wizi vikiwemo vifaa vya maabara, vitabu, kemikali za maabara ya somo la kemia ambavyo vinasadikika  kuwa mali ya shule ya sekondari ya Nyakato iliyopo mjini Bukoba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Philip Kalangi alisema mwishoni mwa wiki katika maeneo ya Uganda  mwalimu Alfred Sitayo (32) mkazi wa kata ya Kibeta alikamatwa akiwa na vifaa mbalimbali vya maabara ambavyo thamani yake bado haijafahamika.

Bw. Kalangi alisema vifaa hivyo vinasadikiwa kuwa ni mali ya shule ya sekondari ya Nyakato , ambapo inadaiwa Bw. Alfred Sitayo alikuwa mwalimu katika shule hiyo kwa upande wa maabara ya kemia kabla ya kuacha kazi.

Alisema baada ya kuacha kazi mwalimu huyo hakukabidhi maabara ya kemia pamoja na vifaa vyake katika uongozi wa shule na kuwa alikamatwa na vifaa hivyo akiwa anavitumia katika kituo chake binafsi ya kufindishia masomo ya ziada tuition.

Aidha alisema polisi wamekamata vifaa mbalimbali vikiwemo komputa, luninga, radio na bangi ambavyo vimekamatwa wakati wa operasheni maalum ya jeshi hilo baada ya kutelekezwa watu wanaosadikiwa kuwa wezi.

mwisho



No comments:

Post a Comment