Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Wednesday, July 11, 2012

BREAKING NEWS KESI YA PROFESA MAHALU IMEAHIRISHWA

Hukumu ya Kesi inayomkabili aliyekuwa balozi wa Tanzania nchia Italia Profesa Costa Mahalu imeahirishwa mpaka tarehe 9 mwezi ujao


Frank Geofray- Jeshi la Polisi, Tabora.
Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa kushirikiana na raia wema wamefanikiwa kuwakamata watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na Mauaji ya Watu wawili ambao ni Mke na Mume tarehe 09 Julai mwaka huu katika Kijiji cha Inala Kata ya Ndevelwa Manispaa ya Tabora.
Watu hao wanatuhumiwa kuwaua kwa kuwakatakata na panga Khalid Said (55) na Amina Ally (50) usiku wa siku hiyo wakati walipokuwa wamepumzika nje ya nyumba yao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi Anthony Rutta aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa kuwa ni Mheshimiwa Shakalambe (55) Mkazi wa Naila, Jumanne Mohamed (30) Msukuma mkazi wa Mbalala Kigwa na Mabula Masanja (33) Msukuma Mkazi wa Mbuyuni Kigwa.
Kamanda Rutta alisema watu hao walikamatwa katika msako mkali uliofanywa na Jeshi hilo mkoani humo ambapo pia wamekutwa na Panga ambalo walilitumia katika kutekeleza mauaji hayo.
“Watu hawa walitumia mbinu ya kujifanya kuwa ni wanunuzi wa Ngo’mbe lakini wakati wakiendelea kujadili biashara hiyo walitokea Vijana wawili ambao kila mmoja wao alikuwa na Panga pamoja na fimbo ndipo wakatekeleza unyama huo na wamedai kuwa waliahidiwa kulipwa milioni moja au Ngo’mbe wawili kwa kazi hiyo”
Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika na Kamanda Rutta ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kukomesha Vitendo vya Mauaji na kuwafichua Wahalifu wa makosa mbalimbali.


Nyanya nyanya tunauza karibu bei kama kawa

No comments:

Post a Comment