Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Wednesday, July 4, 2012

POLISI KAGERA WATUHUMIWA KUVAMIA WANANCHI USIKU NA KUWAVUNJIA NYUMBA ZAO

Askari wa kutuliza ghasia FFU mkoa wa Kagera wakijiandaa katika moja ya shughuli za kuandalia usalama

Na Mwandishi wetu
Bukoba

WANANCHI wa mtaa wa Kyaya katika kata ya Kahororo manispaa ya Bukoba wamelalamikia jeshi la polisi mkoa wa Kagera baada ya polisi kudaiwa kuvamia wakazi wa mtaa huo kuwakamata wakati wa usiku na kisha kuvunja milango na madirisha ya nyumba zao.


 Wakizumgumza mbele ya waandishi wa habari wananchi hao walidai usiku wa kuamkia juzi kati ya saa tano hadi sita askari polisi wakiwa wamevaa za sare za polisi waliwavamia, ambapo walivunja milango, madirisha na kukamata baadhi ya wananchi.

Wananchi hao walisema kitendo cha kuvamiwa na kukamatwa kwao kinatokana mgogoro wa ardhi uliopo baina yao na wamiliki wa shule ya sekondari Nyanshenye ambao unaelezwa kuwepo kwa muda mrefu sasa bila kutatuliwa.

 Kutokana na kitendo hicho wananchi wanadaiwa kukimbia na kutelekeza makazi yao, ambapo wamesema wanalazimika kulala vichakani kwa kuhofia kuvamiwa tena.


Jairos Bulindwi ni miongoni mwa wananchi hao ambaye alishangaa kitendo cha polisi kuwavamia na kuwakamata kama majambazi bila kupita katika uongozi wa mtaa husika, na kuwa kutokana na kitendo hicho kama wananchi wangekuwa na silaha ingewza kuleta matatizo makubwa

 Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Philip Kalangi alikiri wananchi kuvamiwa na kukamatwa kwa madai kwamba walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu sasa.

 Kalangi alisema walikuwa wanatafutwa tangu mwezi Machi baada ya kupewa dhamana na kisha kushindwa kurudi, huku kauli hiyo ikipingwa na wananchi na uongozi wa mtaa husika kwamba hawakuwahi kukamatwa wala kupewa dhamana na jeshi hilo, huku suala la waannchi kuvunjiwa nyumba akihaidi kulizungumzia baada ya kulifanyia uchunguzi.

Mwisho

No comments:

Post a Comment