Na Mwandishi maalum
Bukoba.
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Kagera (TAKUKURU) inawashikilia
watumishi wanne wa serikali kutoka halmashauri ya manispaa ya Bukoba na sekretariti
ya mkoa wa Kagera baada ya kutuhumiwa kujipatia
fedha kwa njia za udanganyifu kwa kupitisha mishahara hewa.
Aidha
TAKUKURU inaendelea kuwasaka watumishi wengine wanne wa halmashauri ya
manispaa ya Bukoba ili waweze kuungana na wenzao katika kujibu tuhuma
hizo.
Kaimu kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Bw. Samsoni
Bishati alisema kuwa watumishi hao wanatuhumiwa kupitisha fedha za mishahara ya watumishi hewa na hivyo kujinufaisha
wao wenyewe.
Miongoni mwa wanaoshikiliwa wawili ni kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa huo ambao ni Shabani Kitimbisi na Sifa Musa wote
wanatoka idara ya uhasibu na fedha.
Bw. Bishati aliwataja wengine kuwa Davidi Buhenyenge
na Martini Muganyizi wote idara ya afya kutoka halmashauri ya manispaa ya
Bukoba na kuwa watumishi wengine wanne kutoka halmashauri hiyo bado wanaendelea
kutafutwa kuhusika na tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment