Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Friday, March 30, 2012

Ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto


MA                 Na Mwandishi wetu
Muleba


    MAHAKAMA ya wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera imemhukumu Samora Theobard (33) mvuvi wa kisiwa cha Bumbile kilichopo wilayani humo, kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa shule ya awali (chekechea).

     Hukumu hiyo ilitolewa juzi ( Machi 28 mwaka huu) na hakimu wa mahakama hiyo Bw. Benedict Nkomola  baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

     Awali ilidaiwa na mwendesha mashtaka mrakibu msaidizi wa polisi Bw. Jumanne Ibrahim mnamo tarehe 21 mwezi Okitoba mwaka jana 2011 saa kumi na moja jioni huko katika kisiwa cha Mchangani Bumbile Samora Theobard alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 6 (jina limehifadhiwa). 

     Bw. Ibrahim alisema mshitakiwa huyo kabla ya kumbaka mwanafunzi huyo wa chekechea alimrubuni kwamba anakwenda kumnunulia biskuti, na hivyo kufanikisha kufanya kitendo hicho, ambacho kilimsababishia maumivu makali.

     Mwisho

No comments:

Post a Comment