Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Saturday, March 24, 2012

RC Massawe awatuhumu viongozi kulinda wafugaji haramu


 Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe akizungumza na wadau wa maendeleo hawapo pichani

Na Mwandishi wetu
Bukoba.

MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe amewatuhumu baadhi ya watendaji ngazi ya mkoa kuwa wanasaliti serikali kwa kushiriki kuwalinda wafugaji haramu kutoka nchi jirani, hali inayoelezwa kukwamisha juhudi za serikali za kuondoa wafugaji hao.

Bw. Massawe alimweleza Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt. Mathayo Devid Mathayo kuwa juhudi za serikali za kuondoa wafugaji haramu linakwamishwa na baadhi ya watendaji kutokana na kile alichodai kuwa wanavujisha taarifa za wafugaji hao kuondolewa kabla ya zoezi husika kufanyika.

Alisema uongozi wa mkoa tayari umeishabaini idadi ya wafugaji haramu na kuwatambua kwa majina pamoja na mahali wanapoishi lakini wanapokaa na kupanga siku maalum ya kuwaondoa wanakuta maeneo yakiwa wazi, ambapo inadai wafugaji hao wanapewa taarifa mapema.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema wanapotoka katika maeneo ya wahamiaji hao haramu wanarejea kwenye makazi yao na kuwa hali hiyo inafanya zoezi la kuwaondoa kuonekana kuwa ngumu.

“Viongozi wengine ni wasaliti wanashirikiana na wahamiaji, na hata humu ndani kuna ma-informer wao (wanaowapatia taarifa za siri) kwani tukipanga kwenda kuwaondoa hatuwakuti tunakuta mazizi ya ng’ombe yakiwa wazi na tukitoka wanarejea hii ni changamoto ” alisema Bw. Massawe.

Akizungumzia sababu ya kushamiri kwa wahamiaji haramu mkoa wa Kagera alisema vijiji vya mipakani kuna watu wanaosaidia kuingiza wageni hao hapa nchini kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji  husika.

Alisema baadhi ya viongozi katika mipaka hiyo sio watanzania, ambapo wanachaguliwa na kuwekwa mipakani kwa ajili ya kulinda maslahi ya wageni kutoka nchi jirani.

Mwisho 


No comments:

Post a Comment