Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Saturday, March 3, 2012

viwanda vya kuchakata samaki hatarini kufungwa

Na Livinus Feruzi Bukoba

SERIKALI isipoongeza nguvu za kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa Victoria, usafirishaji na biashara haramu ya zao la sangara, viwanda vya kuchakata samaki nchini majengo yake yatabakia kumbukumbu na historia ya kuwepo kwa samaki aina ya sangara.

Ofisa mfawidhi wa kikosi cha ulinzi wa raslimali za ziwa kanda ya Kagera Bw. Rodrick Mahimbali anasema kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu katika viwa Victoria .

Anasema uvuvi haramu na usafirishaji wa samaki wachanga ni tishio kubwa kwa ustawi wa raslimali ya uvuvi katika ziwa Victoria hali inayohitaji nguvu za ziada ili kunusuru ziwa hilo ikiwa ni pamoja na maisha ya wananchi wanaotegemea ziwa .

Kauli ya ofisa huyo imekuja siku chache baada ya kukamatwa kwa magari matatu yanayomilikiwa na kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha Vickfish yakiwa na jumla ya kilogramu 614 wa sangara wachanga.

Anasema mbali na ziwa hilo kuwa sehemu mkubwa ya ajira kwa watanzania wengi pia sekta ya uvuvi imekuwa ikiipatia serikali mapato mengi.

Bw. Mahimbali anasema kwa mwaka 2010/2011 mkoani Kagera serikali kuu ilipata zaidi ya milioni 742 fedha ambazo zilitokana na minofu ya samaki ambayo iliuzwa nje ya nchi.

Anasema raia kutoka nchi jirani wamejificha kwenye visiwa mbalimbali vilivyomo ziwa Victoria, ambapo wananunua samaki wachanga na kuwasafirisha kwenda nje ya nchi.

Bw. Mahimbali anasema kikosi cha doria kinashindwa kuendesha doria za mara kwa mara kwenye visiwa vya ziwa victoria mkoa wa Kagera kutokana na fungu dogo linalotolewa , hivyo kupelekea baadhi ya visiwa kutofikiwa na doria hiyo.

Baadhi ya vibarua wakishusha samaki aina ya sangara waliokamatwa katika moja ya gari la kiwanda cha kuchakata samaki cha vicfish, mjini Bukoba mkoa wa Kagera.Sehemu ya mitumbwi na samaki waliokamatwa wakati wa operatisheni maalum iliyoendeshwa na kikosi cha doria kanda ya kagera katika mwalo wa kyandiba uvuvi haramu katika ziwa victoria unahatarisha ustawi wa zao la sangara
1 comment:

  1. kagera ni yetu,ni vyema tukajiepusha na uharifu wa mazao ya majini.

    ReplyDelete