MA Na Mwandishi wetu
Muleba
MAHAKAMA
ya wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera imemhukumu Samora Theobard (33) mvuvi wa
kisiwa cha Bumbile kilichopo wilayani humo, kutumikia kifungo cha maisha jela baada
ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa shule ya awali (chekechea).
Hukumu
hiyo ilitolewa juzi ( Machi 28 mwaka huu) na hakimu wa mahakama hiyo Bw.
Benedict Nkomola baada ya kuridhika na
ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Awali
ilidaiwa na mwendesha mashtaka mrakibu msaidizi wa polisi Bw. Jumanne Ibrahim
mnamo tarehe 21 mwezi Okitoba mwaka jana 2011 saa kumi na moja jioni huko
katika kisiwa cha Mchangani Bumbile Samora Theobard alimbaka mtoto mwenye umri
wa miaka 6 (jina limehifadhiwa).
Bw. Ibrahim alisema mshitakiwa huyo kabla ya kumbaka mwanafunzi huyo wa chekechea alimrubuni kwamba anakwenda kumnunulia biskuti, na hivyo kufanikisha kufanya kitendo hicho, ambacho kilimsababishia maumivu makali.

No comments:
Post a Comment