Sehemu ya nyavu haramu za uvuvi zilizokamatwa na waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt. Mathayo Devid Mathayo katika mwalo wa Ibagiro Bukoba vijijini na kisha kuziteketeza kwa moto. |
Ni rundo la nyavu haramu zilizokamatwa katika mwalo wa Igabiro zikisubiri kuteketezwa kwa moto, nyavu hizi zilikamatwa baada ya ziara ya kushtukiza. |
Mzee huyu anafuatilia jinsi nyavu haramu zinavyoteketea kwa moto, ingawa kuna jua kali lakini anajikinga kwa koti ili ziteketee akiziona kwa macho yake. |
Vijana wa kazi hata nao wapo kwa ajili ya kuangalia usalama kweli wamejiandaa kukabiliana na lolote linaloweza kutokea. |
Na Livinus Feruzi
Bukoba.
Zoezi la kuteketeza nyavu
hizo haramu lilifanyika katika eneo la Kyakailabwa manispaa ya Bukoba, na
kushirikisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa uvuvi nchini Bw. Hoseah
Mbilinyi na mkuu wa mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe.
Awali Ofisa mfawidhi
wa kikosi cha ulinzi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi kanda ya Kagera, Bw.
Rodrick Mahimbali alisema vyavu hizo
zilikamatwa kwa kipindi cha mwaka 2009/10 na mwaka 2010/2011.
Bw. Mahimbali alitaja
zana hizo kuwa ni pamoja na kokoro 503, timba 785, makila 12,965, nyavu za
dagaa na kamba za kuvutia kokoro zenye urefu wa mita 192,274, ambapo alisema
kukamatwa kwa zana hizo kulitokana na ushirikiano baina ya kikosi hicho na
wadau mbalimbali.
Alisema nyavu hizo zilikamatwa kwenye mialo mbalimbali ya
ziwa Victoria, vituo vya mabasi, maghala, vyombo vya uvuvi na katika makazi ya
wananchi na kuwa baada ya kukamatwa zilihifadhiwa katika ofisi ya doria
zikisubiri kuteketezwa.
“Kwa miaka miwili
iliyopita kikosi cha ulinzi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi kanda ya Kagera
zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 na kuzihifadhi zikisubiri
kuteketezwa mheshimiwa waziri tunaomba siku ya leo uteketeze nyavu hizi”
alisema Bw. Mahimbali.
Mbali na kuteketezwa nyavu hizo zilizokamatwa na kikosi cha doria pia Waziri Mathayo juzi
aliteketeza vyavu zinazokadiriwa kufikia 1,000 ambazo alizikamata mwenyewe
wakati wa ziara ya kushtukiza katika mwalo wa Igabiro uliopo Bukoba vijijini.
Hata hivyo pamoja na
mambo mengine Dkt. Mathayo aliwataka wavuvi nchini kutambua madhara ya uvuvi
haramu huku wakiwatahadharisha kuwa wasipoacha uvuvi haramu kuna hatari ya
samaki katika ziwa Victoria
kubaki historia ikiwemo wananchi kukosa kipato.
Mwisho
No comments:
Post a Comment