Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe akizungumza na wadau wa maendeleo hawapo pichani
Na Mwandishi
wetu
Bukoba.
MKUU wa mkoa
wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe amewatuhumu baadhi ya watendaji ngazi
ya mkoa kuwa wanasaliti serikali kwa kushiriki kuwalinda wafugaji haramu kutoka
nchi jirani, hali inayoelezwa kukwamisha juhudi za serikali za kuondoa wafugaji
hao.
Bw. Massawe
alimweleza Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt. Mathayo Devid Mathayo
kuwa juhudi za serikali za kuondoa wafugaji haramu linakwamishwa na baadhi ya
watendaji kutokana na kile alichodai kuwa wanavujisha taarifa za wafugaji hao
kuondolewa kabla ya zoezi husika kufanyika.
Alisema
uongozi wa mkoa tayari umeishabaini idadi ya wafugaji haramu na kuwatambua kwa
majina pamoja na mahali wanapoishi lakini wanapokaa na kupanga siku maalum ya
kuwaondoa wanakuta maeneo yakiwa wazi, ambapo inadai wafugaji hao wanapewa
taarifa mapema.
Hata hivyo
mkuu huyo wa mkoa alisema wanapotoka katika maeneo ya wahamiaji hao haramu
wanarejea kwenye makazi yao na kuwa hali hiyo inafanya zoezi la kuwaondoa
kuonekana kuwa ngumu.
“Viongozi
wengine ni wasaliti wanashirikiana na wahamiaji, na hata humu ndani kuna
ma-informer wao (wanaowapatia taarifa za siri) kwani tukipanga kwenda kuwaondoa
hatuwakuti tunakuta mazizi ya ng’ombe yakiwa wazi na tukitoka wanarejea hii ni
changamoto ” alisema Bw. Massawe.
Akizungumzia
sababu ya kushamiri kwa wahamiaji haramu mkoa wa Kagera alisema vijiji vya
mipakani kuna watu wanaosaidia kuingiza wageni hao hapa nchini kwa kushirikiana
na viongozi wa vijiji husika.
Alisema baadhi
ya viongozi katika mipaka hiyo sio watanzania, ambapo wanachaguliwa na kuwekwa
mipakani kwa ajili ya kulinda maslahi ya wageni kutoka nchi jirani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment