Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Monday, May 27, 2013

HALMASHAURI MANISPAA YA BUKOBA WAKO WAPI?


Takataka katika dampo la Kashai zinahatarisha afya za wananchi wa kata ya Kashai, ni hatua chache kutoka katika dampo hilo hadi kufikia sehemu pa kuuzia chakula (vibanda vya mamalishe)  na sehemu pa kuuzia samaki.

 
Pamoja na mlundikano wa takataka hizo ambazo zimepelekea baadhi ya wafanyabaishara kukimbia maeneo hayo kutokana na harufu mbaya, wateja wachache wanaopita eneo hilo bado wanaendelea kuangalia sample mbalimbali za nguo.


Mlundikano wa takataka katika soko la Kashai, ambazo zinahatarisha usalama wa wafanyabiashara ndogondogo wa nguo, kutokana na takataka hizo wafanyabiashara hao wanalalamikia kupungua kwa wateja kutokana na harufu mbaya. 


Baadhi ya wapita njia wakipata shida kupita kwenye eneo la soko  la Kashai ambalo kwa sasa takribani miezi mitatu takataka hizo hazijatolewa na kusababisha kuziba njia na kubanda vya wauza nguo, hata hivyo wafanyabaishara hao wanalazimika kusubiri wateja wakiwa mbali na vidanda vyoa kutokana na harufu mbaya.
  
Hali halisi ilivyo katika soko la Kashai

Kwa harufu hii tunapita kwa sababu hatuna sehemu nyingine pa kupita.
 
Baadhi ya wapita njia wakipata shida kupita kwenye eneo la soko  la Kashai, wafanyabiashara wanasema iko hatari ya kuugua magonjwa ya tumbo hususan kipindupindu kwani  tangu kulundikwa kwa takataka hizo wamekuwa wakisumbuliwa na matumbo.


No comments:

Post a Comment