Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Monday, May 6, 2013

MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI MULEBA

 Mkuu wa wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo akifafanua jambo wakati akiwahutubia madiwani, watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Muleba alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la madiwani.

Mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya ya Muleba George Katomero akifungua mkutano wa baraza la madiwani pembeni mwake ni mkurugenzi mtendaji wa halamshauri hiyo Oliver Vavunge na makamu mwenyekiti Swaibu Mfuruki.

 Baadhi ya madiwani wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa baraza la madiwani, kulia ni diwani wa kata ya Gwanseli Julius Rwakyendera.
 Diwani wa kata ya kamachumu Danstan Mutagahywa akijiandaa kuchangia mada wakati wa mkutano wa baraza la madiwani
Diwani wa Muhutwe Justus Magongo akipitia nyaraka mbalimbali kabla ya kuchangia hoja.
madiwani, watendaji na wageni waalikwa wakiimba wimbo wa mkoa kabla ya kuanza kwa mkutano wa baraza, katika shughuli mbalimbali wimbo wa mkoa unaimbwa kabla ya shughuli husika kuanza


No comments:

Post a Comment