Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Friday, May 10, 2013

UPATIKANAJI WA SENENE KWA SIKU YA LEO MJINI BUKOBA ......


Mifuko ya senene ikiwa katika eneo la soko kuu mjini Bukoba kusubiri wateja kwa ajili ya kununua kitoweo hicho muhimu kwa wakazi wa mkoa wa Kagera na hata nje ya mkoa ambacho ni adimu kupatikana kwake.senene wakiwa kwenye mfuko eneo la soko kuu kusubiri wateja

Wananchi kutoa maeneo mbalimbali wakimiminika katika eneo la soko kuu la mjini Bukoba kwa ajili ya kununua senene ambao walioneka kuwa wengi siku ya leo tafauti na siku kadhaa zilizopita, huu ndo msimu ya kuvuna senene.


Kutokana na wingi wa watu waliojaa katika eneo la soko kuu kwa ajili ya kununua au kuuza senene, imepelekea eneo hilo kuwa na msongamano wa magari, pikipiki na baiskeli na hivyo kusababisha usumbufu kwa wapita njia.


No comments:

Post a Comment