Matangazo yanakaribishwa katika blog hii,piga simu no 0753 239 687 Email-livinusferuzi@yahoo.com

Friday, May 10, 2013

POLISI KAGERA YAWANASA WATUHUMIWA NANE WA UJAMBAZI SUGU


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe akionyesha bunduki na risasi zilizokamatwa.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe akionyesha bunduki iliyokamatwa.


Bunduki moja aina ya SMG na risasi 16 iliyokamatwa
 Na Mwandishi wetu
Bukoba.

POLISI mkoani Kagera wamewakamata watu wanane wanaosadikiwa kuwa ni majambazi sugu, ambao wamekuwa wakitafutwa kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo utekaji wa magari maeneo ya porini na uporaji wa mali za wafanyabiashara.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe anasema kwa muda mrefu polisi wamekuwa wakifuatilia mtandao wa majambazi wanaojificha katika mapori, ambapo huteka magari na kupora mali za wafanyabiashara.

Anawataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na mwanamke mmoja Leoncia Rovast (28), ambaye anadaiwa kuwa kinara wa kupanga mipango ya utekaji na uporaji.

Watuhumiwa wengine kuwa ni Iman Ezekiel (24), Ndanda Iliofu (24), Hanana Francis A.KA Baseka (26) Kabichi Sylivestar (23), Slambuki Abel (25) na Amos Amos (30) A.K.A Rasi.

Wengine ni Sabuhalo Daud (26) ambaye anatuhumiwa kuhusika na utunzaji wa mali na vifaa vinavyoporwa baada ya utekaji, ambapo alikutwa na bunduki moja aina ya SMG na risasi 16.

mwisho

No comments:

Post a Comment